Je, mbio za ubingwa wa Ligi Kuu zimesalia na timu mbili baada ya mechi 11 pekee za msimu huu?Viongozi Liverpool walipata ufanisi wikendi baada ya ushindi dhidi ya Aston Villa pamoja na kushindwa kwa Manchester City dhidi ya Brighton - na sare ya 1-1 Jumapili kati ya Arsenal na Chelsea.Sasa wanaongoza City kwa pointi tano - na waliosalia na pointi tisa au zaidi.
'Kompyuta ya Opta inaipa Arsenal ya Mikel Arteta 3.5% ya nafasi ya kushinda ubingwa, huku Chelsea ikiwa chini kwa 0.2% na timu nyengine yoyote ikiwa chini ya takwimu hiyo.
"Singemwacha mtu yeyote ambaye yuko juu ya jedwali kwa sasa," mchambuzi wa MOTD2 na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Theo Walcott anasema.
"Liverpool wakati fulani itajikwaa na watakuwa na matatizo ya majeraha kama timu nyingine."
Hata hivyo, akiongea kwenye MOTD2, mshambuliaji wa zamani wa Premier League Troy Deeney alionya: “Wakipoteza mara moja zaidi nadhani Arsenal watakuwa wamejiondoa. Watalazimika kuifunga Liverpool nyumbani na ugenini na kuifunga City pia."
Je, Arsenal wametoka kwenye mbio za kuwania ubingwa?
Mashabiki wa Arsenal walitarajia huu utakuwa msimu wao baada ya kuisukuma Manchester City katika misimu miwili iliopita .
Na huku City ikiyumba - baada ya kushindwa mara nne mfululizo katika mashindano yote - hii inaweza kuwa nafasi yao nzuri.
Lakini Liverpool wanafanya vizuri zaidi kuliko ambavyo mtu yeyote angefikiria chini ya kocha mpya Arne Slot, wakiwa na pointi 28 kati ya 33.
The Gunners walijipata nyuma kwa pointi tisa mwishoni mwa wikendi kwa mara ya kwanza tangu 2021-22, walipomaliza kwa pointi 24 nyuma ya Manchester City.
Walionekana kuhuzunika huku kipenga cha mwisho kikipulizwa uwanjani Stamford Bridge.
Walcott anasema: "Tofauti na Arsenal ya sasa ni kwamba wanakosa mabao, huku wakiwa hawafungi mabao mengi - lakini kwa wakati huu wa msimu ni muhimu kuzingatia ni nani wamecheza nao.
"Naweza kusema kwamba, hadi sasa, wamecheza dhidi ya timu ngumu zaidi - wamecheza na timu sita kati ya 10 bora za msimu uliopita, na tano kati ya mechi hizo wamecheza ugenini.
"Pamoja na hayo, muda mwingi wamekuwa bila mchezaji wao mkuu, Martin Odegaard, na bado wako hapo walipo."
Nahodha Odegaard alicheza mechi yake ya kwanza ya Premier League tangu Agosti dhidi ya Chelsea na kutengeneza bao la ufunguzi la Gabriel Martinelli.
Walcott aliongeza: "Watu huwa wanasahau yote hayo wanapoangalia jinsi Arsenal ya sasa katika kiwango sawa na ilivyokuwa mwaka jana, lakini kwangu mimi ni moja ya sababu za kutokuwa kwenye mbio za ubingwa."
Mchezaji wa zamani wa Gunners Paul Merson, akizungumza kwenye Sky Sports, alisema: "[Arteta] lazima ahakikishe tofauti yake na kiongozi wa jedwali ni pointi sita badala ya 12.
"Nadhani watafanya vyema iwapo wataifikia Liverpool. Inaweza kusalia pointi tisa hadi mwisho wa Desemba."
Arsenal wanaweza kufanya hivyo? Kweli, historia haiko upande wao.
Ukiondoa timu zilizo na mechi mkononi, hakuna aliyewahi kushinda taji la Ligi Kuu baada ya kuwa na pointi tisa (au zaidi) kileleni huku mechi 11 zikiwa zimepita.
Manchester City ilifanikiwa msimu wa 2013-14 lakini vinara Arsenal walikuwa wamecheza mechi 12 kufikia hatua hiyo.
Akizungumzia kuhusu washindani wake, Arteta alisema timu yake inahitaji "kushinda, kushinda, kushinda, kushinda na kushinda, kwa sababu watu hawa hawaachi kushinda".
Iwapo wangeshinda kila mechi iliyosalia msimu huu wangemaliza wakiwa na pointi 100, huku kiwango cha sasa cha Liverpool kikiwaweka kwenye mstari wa kufikisha pointi 97.
Je, liverpool ina kila uwezo wa kushinda taji hilo?
Liverpool ni timu ya sita tu katika historia ya Premier League kuwa mbele kwa pointi tano baada ya mechi 11.
Timu zote tano zilifanikiwa kushinda taji - ikiwa ni pamoja na Liverpool mnamo 2019-2020, mara ya mwisho timu ilikuwa mbele katika hatua hii.
Kulikuwa na wasiwasi mwingi kuhusu jinsi Liverpool ingeendelea baada ya kuondoka kwa kocha maarufu Jurgen Klopp msimu uliopita - lakini wanaendelea kung'aa chini ya Slot.
Kiungo wa kati wa Reds Alexis Mac Allister alisema "kabla ya msimu kuanza singesema tulikuwa wagombea, lakini sasa inaonekana kama [sisi]" baada ya ushindi wao wa 2-0 dhidi ya Villa.
Opta inawapa nafasi ya 58.3% ya ubingwa - kutoka 5.1% kabla ya msimu.
Walcott alisema: "Kile Liverpool wamepata ni kwamba wana idadi kubwa ya mabao kwenye timu yao. Ukiangalia tofauti yao ya mabao ukilinganisha na timu nyengine ni kubwa.
"Kwa hivyo haijalishi kama wataanza kuruhusu mabao, kwa sababu wanaweza kukuzidi.
Je, matumaini ya City yakoje?
Pep Guardiola amepoteza michezo minne mfululizo katika mashindano yote kwa mara ya kwanza (bila kujumuisha mikwaju ya penalti) katika maisha yake ya soka ya Barcelona, Bayern Munich na City.
City wanawania kushinda taji la tano la Ligi Kuu ya Uingereza - lakini Opta inawapa nafasi ya 38% ya kufanya hivyo. Idadi hiyo ilikuwa 82% kabla ya msimu huu.
"Labda baada ya miaka saba kushinda Ligi Kuu sita, pengine timu nyingine inastahili," alisema Guardiola.
Hatahivyo, ni wamalizaji wazuri na wamepoteza mechi nne pekee za Ligi Kuu baada ya Krismasi katika misimu mitatu iliyopita.
Zaidi ya hayo wameshinda vikwazo vikubwa zaidi kuliko nakisi ya pointi tano baada ya mechi 11.
Vipi kuhusu Chelsea na timu nyengine?
Chelsea, ambao wako katika nafasi ya tatu, Brighton na Nottingham Forest wote wako sawa kwa pointi 19 na Arsenal walio nafasi ya nne.
The Blues haikutarajiwa kushindania taji msimu huu, baada ya kumaliza katika nafasi ya sita muhula uliopita kabla ya msimu mwingine wa kiangazi wa kujenga upya.
Chelsea ilimaliza siku katika timu tatu bora za Premier League kwa mara ya kwanza tangu siku ya mwisho ya msimu wa 2021-22, ilipomaliza katika nafasi ya tatu nyuma ya Manchester City na Liverpool.
Bosi Enzo Maresca alisema baada ya bao la kusawazisha la Pedro Neto dhidi ya Arsenal kwamba timu yake iko mbele ya ratiba.
"Kwangu mimi tuko nyuma ya City na Arsenal," kocha msaidizi wa zamani wa City alisema.
"Kila siku wanafanya kazi pamoja na meneja mmoja kwa miaka tisa iliyopita. Haimaanishi kwamba hatutajaribu kushinda. Sisi ni moja ya timu kubwa duniani."
Licha ya mwanzo mzuri wa Brighton, ambao waliwashinda City, na Forest - ambao walipoteza kwa Newcastle siku ya Jumapili - hakuna ambaye amezungumza juu yao katika suala la ubingwa.
0 Comments