Ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Ireland unamfanya kocha wa mpito wa Uingereza Lee Carsley kuendelea kufanya vyema katika kibarua chake tangu akabidhiwe kibarua majukumu mwezi Agosti. Carley alichukua mikoba ya Gareth Southgate aliyeamua kujiuzuru. Kocha Lee Carley ameiongoza Uingereza katika michezo 6 na kuibuka na ushindi wa mechi 5 mchezo mmoja akipoteza.
Katika mchezo dhidi ya Ireland kocha Lee Carsley alianza na Pickford ,Livrante,walker,Guehi,Hall,Garagher,Jones,Madueke,Bellingham ,Gordon na Harry Kane. Na wafungaji katika mchezo huo ni Harry Kane dakika ya 53 kwa mkwaju wa Penati,Gordon dakika ya 55 ,Conor Gallagher dakika ya 58 na nyota Bowen na Bellis wakitokea sub walifunga mabao dakika ya 76 na 79. Wengi wanaamini ushindi wa Uingereza ulitokana na kadi nyekundu aliyopata beki wa kati Liam Scales dakika ya 51 wakati huo timu hizo zilikuwa hazijafungana.
Lee Carley atakabidhi majukumu ya ukocha kwa Tomas Tuchel aliyetangazwa kama mrithi sahihi wa Gareth Southgate na kocha huyo ataiongoza uingereza katika mbio za kutwaa ubingwa wa dunia nchini Marekani mwaka 2026.
0 Comments