Baada ya Shamra Shamra za wikiendi ya ligi kuu NBC kumalizika na kushuhudia Steven Mukwala akiwapa Simba SC alama tatu kwa bao lake la kichwa na kuwafanya waendelee kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kwa kufikisha alama 22 ,mambo yalikuwa mabaya kwa wapinzani wao wa jadi Yanga ambao walipoteza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu msimu huu dhidi ya Azam FC kwa bao murua lililofungwa na DJibril Silla.
Ushindi wa bao 1-0 unawafanya azam kufikisha alama 21 wakishika nafasi ya 4 wakiweka matumaini ya kutwaa ubingwa msimu kwani Yanga wanaoongoza kwa alama 24 hivyo tofauti ya alama 3 ni fursa kwa azam kufikia malengo yake .
BLUE FOOTBAL MONDAY
TABORA UNITED VS MASHUJAA
Ligi kuu ya NBC inaendelea leo hii kwa kuwakutanisha Tabora United dhidi ya Mashujaa mchezo utakaopigwa majira ya saa 10 jioni.Mashujaa wametoka kupoteza mchezo dhidi ya Simba SC siku ya ijumaa kwa bao lililofungwa na Steven Mukwala dakika ya 90+8 na kuwafanya kusalia na alama 13 katika michezo 9 ya ligi wakiwa nafasi ya 7 . Kama wataibuka na ushindi kwenye mchezo huo basi watarejea afasi ya 6 inayokaliwa na KMC wenye alama 14.
Tabora United wanashika nafasi ya 10 wakiwa na alama 11 katika michezo 9 waliyocheza mpaka sasa. Mchezo wa mwisho kwa Tabora ulikuwa dhidi ya Pamba jiji tarehe 23 oktoba na waliibuka na ushindi wa 1-0 hivyo wamepata wasaa mzuri wa kujiandaa na mchezo huo muhimu. Kama wataibuka na ushindi katika mchezo huo watafikisha alama 14 na kupanda mpaka nafasi ya 8 kwenye msimamo wa ligi.
KAGERA SUGAR VS DODOMA JIJI
Kagera Sugar wamejipambanua upya tangu wamkabidhi timu kocha Melis Medo ameingoza timu hiyo katika michezo miwili akipata sare ya mabao 1-1 dhidi ya Pamba Jiji na kupoteza mchezo kwa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union.Kagera wameanza vibaya msimu huu baada ya kuvuna alama 5 pekee kwenye michezo 9 na kuangukia katika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi. Wanakwenda kucheza na timu ngumu ya Dodoma Jiji ambao kwa sasa wamekusanya jumla ya alama 13 katika michezo 10 waliyocheza.
Endapo Kagera wataibuka na ushindi katika mchezo huo watafikisha alama 8 na kuendelea kusalia nafasi ya 14 tofauti na Dodoma jiji ambao kama wataibuka na ushindi basi watasogea mpaka nafasi ya 6 wakiwa na alama 16 na huo utakuwa ni mwendelezo mzuri kwa kocha Mecky Mexime katika mbio zake za kumaliza nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi
0 Comments