Marseille iliishinda Nantes mabao 2-1 na kukwea hadi nafasi ya pili ya Ligue 1 ikiwa na jumla ya pointi 20, na kuwaweka pointi sita pekee nyuma ya nafasi ya kwanza, huku wenyeji wakikaribia eneo la kushushwa daraja kwa hatari.
Kipindi cha kwanza kilianza huku Marseille wakithibitisha mamlaka yao, walianza kupata bao dakika ya 24 kwa bao la Neal Maupay. Hata hivyo, Tino Kadewere alisawazisha dakika ya 39 na kupelekea mchezo kwenda mapumziko.
Kipindi cha pili, Mason Greenwood aliifungia Marseille bao la ushindi dakika ya 61, kwa mwendo wa kustaajabisha ambao ulimshinda mlinda mlango wa timu pinzani. Kwa kufanya hivyo, timu hiyo ilinyakua nafasi ya pili kwenye ligi, na kuwazidi Monaco kwa tofauti ya mabao.
Greenwood alijiunga na Marseille wakati wa majira joto na amefanikiwa kufunga mabao 7 katika mechi 10 za Ligue 1 akichangia upatikanaji wa bao 1.,Nyota huyo mwenye miaka amekuwa na mwendelezo mzuri tangu atue klabuni hapo akiwa na uwezo wa kucheza nafasi zote tatu za ushambuliaji akicheza kama winga wa kulia na kushoto au mshambuliaji wa kati .
Itakumbukwa nyota huyo aliondoshwa manchester United kwa kile kinachodaiwa ni udharirishaji kwa wanawake baada ya aliyekuwa mpenzi wake kumshtaki. Nyota huyo alikaa nje ya uwanja kwa wuda wa mwaka mmoja kisha baadaye alitangazwa kusajiliwa na Olympic Marseille ya Ufaransa
0 Comments