BETI NASI UTAJIRIKE

ZAHERA AMEKALIA KUTI LAMOTO

 Klabu ya Namungo imeendelea kufanya vibaya mechi za ligi kuu ya NBC baada ya kukubali kipigo cha tatu kutoka kwa Dodoma jiji. Paul Peter ndiye aliyefunga bao la Dodoma jiji dakika ya Kwanza ya mchezo na bao hilo lilidumu mpaka dakika ya tisini .

Dodoma jiji imevuna jumla ya alama 5 katika mechi tatu walizocheza wakipata sare mbili na ushindi wa mechi 1. Kwa upande wa Namungo jahazi limezidi kuzama baada ya kufungwa mechi 3 mfululizo.

Namungo walipoteza mchezo wao wa Kwanza dhidi ya Tabora United wakapoteza mchezo dhidi ya Fountain gates na sasa wamepoteza kwa Dodoma jiji. Namungo wanashikilia mkia wa msimamo wa ligi.

 Siku chache zilizopita timu hiyo ilimwongeza Ngawina Ngawina kuwa kocha msaidizi akiisaidiana na Mwinyi Zahera.ujio wa Ngawina Ngawina haujaleta matokeo chanya na kuna uwezekano mkubwa kocha Mwinyi Zahera akafungashiwa vilago siku za hivi karibuni na nafasi Yake kuchukuliwa na Juma Mgunda au Ngawina Ngawina.

Post a Comment

0 Comments