Timu ya Tanzania,Taifa Stars imeendelea kufanya vyema hatua za makundi kufuzu AFCON 2025 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Guinea. Guinea walikuwa wa kwanza kupata bao la uongozi lililofungwa na Mohammed Bayo dakika ya 57 .Mabao ya Stars yaliwekwa kimiani na Feisal Salum dakika ya 61 kwa shuti la nje ya box lililomshinda golikipa wa Guinea. Mudathir Yahya alifunga bao la pili dakika ya 88 na kuifanya Stars kutoka kifua mbele kwenye mchezo huo.
Kocha Hemed Suleiman alifanya mabadiliko madogo kwenye kikosi kilichoanza dhidi ya Guinea kwa kuanza na Ally Salim,Lusajo Mwaikenda,Mohammed Husein ,Ibrahim Abdulla,Dickson Job,Novatus Dismas ,Edwin Balua,Mudathir Yahya,Feisal Salum ,Wazir Junior na Clement Mzize.
Ushindi huo unaifanya Stars kuwa na alama 4 kwenye kundi H ikishika nafasi ya pili nyuma ya DR Congo wenye alama 6 kwenye michezo miwili waliyocheza. Stars imeendelea kujiweka kwenye nafasi nzuri na mchezo ujao itavaana na DR Congo uwanja wa Benjamin Mkapa.
Mara baada ya mchezo kumalizika Feisal Salum aliyefunga bao alinukuliwa akisema
'' Mchezo ulikuwa mgumu hasa ugenini,Mwalimu alinipa maelekezo kwamba nikifika karibu na golini nijaribu kupiga mashuti na kufanikiwa kupata bao,nadhani mwalimu aliniambia vile kwa sababu anaujua uwezo wangu. Tunawaomba watanzania waaendelee kutusapoti hii ni timu yao ya Taifa''
Naye Mudathir Yahya aliyefunga bao alinukuliwa akisema
''Najiskia Faraja kubwa na nawapongeza wachezaji wenzangu kwa mchezo mzuri waliouonyesha ukatupa ushindi pili tumecheza na timu ngumu na yenye wachezaji wengi wanaocheza nje ya nchi .Kwetu wachezaji wanaotoka nje ni Himid Mao na Novatus Dismass.JapoWatanzania wenzetu wanatubeza ,lakini tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hali hii.Ile simu ni kwa President Kalia pamoja na mama Samia Suluhu Hassan''
0 Comments