Antony anataka kupigania nafasi yake Manchester United licha ya kuhusishwa na Fenerbahce, vilabu vyote vinne vya Uturuki vinavyomlenga Kieran Trippier vimemaliza harakati zao kumsajili, Aston Villa ilikataa ofa 40 za kumtaka Jhon Duran.
Winga wa Brazil Antony, 24, anasita kuondoka Manchester United licha ya Fenerbahce kumtaka . (ESPN)
Vilabu vya Super Lig vya Uturuki Istanbul Basaksehir, Fenerbahce, Besiktas na Eyupspor vimekata tamaa kujaribu kumsajili Kieran Trippier baada ya Newcastle kuweka wazi kuwa wanataka kusalia na beki huyo wa zamani wa Uingereza, 33. (Sky Sports).
Aston Villa walimthamini sana Jhon Duran hivi kwamba walikataa ofa 40 kwa mshambuliaji huyo wa Colombia mwenye umri wa miaka 20 katika msimu wa joto. (Mirror)
Meneja wa Newcastle Eddie Howe na mkurugenzi wa michezo Paul Mitchell wametatua tofauti zao na sasa wanaangazia uhamisho wa Januari, ikiwa ni pamoja na kumleta beki wa Crystal Palace wa Uingereza Marc Guehi, 24. (Telegraph - usajili unahitajika, nje)
Manchester United wanamfuatilia beki wa kulia wa Sevilla, Juanlu Sanchez, 21. (AS - kwa Kihispania)
Real Madrid pia wanavutiwa na Sanchez.(Teamtalk)
Chelsea wamefanya mazungumzo kuhusu kuondoka Stamford Bridge na kujenga uwanja mpya katika Earl's Court. (Guardian)
Tottenham ilikataa ofa za kumnunua beki wa Argentina, Cristian Romero, 26, wakati wa dirisha la uhamisho wa wachezaji kutoka Manchester United , Real Madrid na Paris St-Germain . (TyC Sports, kupitia Mail)
Beki wa Scotland Liam Cooper, 33, anakaribia kujiunga na CSKA Sofia kwa uhamisho wa bila malipo baada ya kuondoka Leeds mwishoni mwa msimu uliopita. (Football Insider)
Mfanyabiashara wa Marekani John Textor ana imani kuwa dili la kuinunua Everton linaweza kukamilika baada ya wiki nne. (Guardian)
Andy Mangan wa Stockport County amezuiwa kujiunga na timu ya makocha ya Real Madrid baada ya kunyimwa kibali cha kufanya kazi kwa sababu ya kanuni za Brexit. (Times - usajili unahitajika)
Galatasaray wana nia ya kumsajili winga wa Chelsea mwenye umri wa miaka 20 kutoka Uingereza Carney Chukwuemeka kwa mkopo.(Teamtalk)
0 Comments