BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA USAJILI DUNIANI LEO 09 AGOSTI 2024

 Mkataba wa nahodha wa Liverpool Virgil van Dijk unamalizika msimu ujao wa joto na mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi, 33, anasema anataka kusaini mkataba mpya wa kusalia katika klabu hiyo hadi Kombe la Dunia la 2026. (Mirror)



Arsenal haiko tayari kumruhusu kiungo wa kati wa Italia Jorginho kuondoka katika klabu hiyo, licha ya kwamba Galatasaray inaripotiwa kutaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 kabla ya dirisha la usajili la Uturuki kufungwa.(Talksport)

Barcelona wanalenga mlinzi wa Bayer Leverkusen Jonathan Tah, 28, na beki wa kulia wa Bayern Munich Joshua Kimmich, 29, ambao wote wanachezea Ujerumani, huku kukiwa na sintofahamu kuhusu mustakabali wa beki wa Uruguay Ronaldo Araujo, 25, na kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong. , 27, katika Nou Camp. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania),

Atletico Madrid, Barcelona na Juventus ni miongoni mwa vilabu vinavyomtaka kiungo wa kati wa Ghana na Arsenal Thomas Partey, 31 .(Caught Offside)

Paris St-Germain wanashughulika kuongeza mkataba wa meneja Luis Enrique, ambao kwa sasa unaendelea hadi Juni 2025. (Fabrizio Romano)

Mshambulizi wa Canada Jonathan David, ambaye alihusishwa na Chelsea katika majira ya joto, amesema alifanya mazungumzo na "timu kadhaa" lakini alichagua kusalia Lille. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliongeza kuwa sasa anajadili kuongeza kandarasi yake zaidi ya msimu ujao wa kiangazi na klabu hiyo ya Ufaransa. (Athletic),

th

Manchester United na Newcastle United wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 29, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Juventus msimu wa joto(Caught Offside)

Mkurugenzi wa zamani wa michezo wa Newcastle United , Dan Ashworth, ambaye sasa yuko Manchester United, amekwazwa na shutuma kutoka kwa Paul Mitchell, mrithi wake katika klabu ya St James' Park, ambaye amesema muundo wa klabu hiyo wa uhamisho "haufai kwa malengo" ya kilabu (Telegraph)

Fenerbahce wamekubali mkataba wa kumsaini winga wa Serbia Filip Kostic, 31 kutoka klabu ya Italia Juventus. (Tuttosport - kwa Kiitaliano)

Fowadi wa Uholanzi Memphis Depay, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Atletico Madrid, amekamilisha uchunguzi wa kimatibabu na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 sasa anatazamiwa kusaini mkataba hadi 2026 na klabu ya Corinthians ya Brazil. (Fabrizio Romano)

Post a Comment

0 Comments