BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA USAJILI DUNIANI LEO 05 SEPTEMBA 2024

 Mchezaji wa Manchester City na Uhispania Rodri, 28, anasakwa na Real Madrid, ambao wanapanga kumnunua kiungo huyo mwishoni mwa msimu huu. (AS – In Spanish)


Istanbul Basaksehir ni moja ya klabu vnne za Uturuki ambazo zimetoa ofa ya mkopo kwa Newcastle ikiwa na chaguo la kumnunua beki wa zamani wa Uingereza Kieran Trippier, 33. (Sky Sports)

Galatasaray wanavutiwa na mkataba wa mkopo wa kiungo wa kati wa Brazil Casemiro, 32, lakini Manchester United italazimika kufidia baadhi ya mshahara wake wa pauni 300,000 kwa wiki. (Times – Subscription Required)

.

Klabu za Saudi Pro League pia zinaweza kutaka kumnunua kiungo huyo kwa bei iliyopunguzwa Januari. (iSport),

Casemiro anatazamiwa kukataa kuhamia sehemu nyingine kwani amedhamiria kupigania nafasi yake United. (Mail)

Newcastle wamesitisha harakati zao za kumtafuta beki wa Crystal Palace, 24, Muingereza, Marc Guehi, ili kuonyesha kuwa klabu hiyo haitatumiwa kufurahisha wengine wakati wa dirisha la uhamisho. (Telegraph – Subscription Required)

.

Beki wa Real Madrid na Uhispania Dani Carvajal, 32, anasema kwamba huenda akacheza nchini Marekani kabla ya mwisho wa maisha yake ya uchezaji. (Athletic – Subscription Required)

Everton wanafikiria kumteua tena David Moyes kama meneja – miaka 11 baada ya Mskoti huyo kuondoka Goodison Park na kuinoa Manchester United. (Football Insider)

Roma wanajiandaa kumsajili beki Mjerumani Mats Hummels, 35, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Borussia Dortmund. (Subscription required)

Post a Comment

0 Comments