BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA USAJILI DUNIANI LEO 04 SEPTEMBA 2024

 Galatasaray wapo kwenye mazungumzo na Manchester United kuhusu uhamisho wa mkopo wa mwaka mmoja kwa kiungo wao wa kati wa Brazil Casemiro, 32. (Ali Naci Kucuk – In Turkish),


Liverpool wanapanga kufanya mazungumzo ya kandarasi na mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 32, baada ya kusema huu ulikuwa “msimu wake wa mwisho” katika klabu hiyo kufuatia ushindi wao dhidi ya Manchester United. (Football Insider)

Meneja wa Pumas UNAM Gustavo Lema anasema Liverpool ilijaribu kumsajili winga wao wa Mexico Cesar Huerta, 23. (TUDN – In Spanish}

Chelsea wako tayari kumtuma beki wa kushoto wa Uingereza Ben Chilwell, 27, kwa mkopo Uturuki, ingawa bado hawajapokea ofa yoyote. (Telegraph – Subscription Required)

Mazungumzo yanaendelea kati ya Chelsea na AEK Athens kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wa Ivory Coast David Datro Fofana, 21. (Mail)

Tottenham wamefanya mazungumzo ya kumnunua kiungo wa kati wa Marekani Johnny Cardoso, 22, kwa £21m kutoka Real Betis. (Telegraph – Subscription Required)

Kiungo wa kati wa zamani wa Liverpool Naby Keita, 29, yuko kwenye mazungumzo na Istanbul Basaksehir kuhusu uwezekano wa kuhama kutoka Werder Bremen baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Guinea kutokubaliana na masharti ya kuhamia Sunderland. (Guardian).Winga wa zamani wa Manchester United Anthony Martial, 28, amepewa mkataba na AEK Athens ambao utamfanya kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi klabuni hapo. Mfaransa huyo alikua mchezaji huru wakati kandarasi yake United ilipoisha mwezi Juni. (Sport24 via Sun).

Manchester United inamfuatilia kwa karibu beki wa kushoto wa Juventus mwenye umri wa miaka 23 kutoka Colombia Juan Cabal. (Tutto Juve – In Italy), nje

Real Betis walitoa ofa kwa kiungo wa kati wa Manchester United na Denmark Christian Eriksen, 32, siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho (Fabrizio Romano)

Post a Comment

0 Comments