BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA USAJILI DUNIANI LEO 01 SEPTEMBA 2024

 Liverpool ilichunguza uwezekano wa kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Nigeria Victor Osimhen, 25, katika dirisha la usajili la kiangazi lakini wakakatishwa tamaa na mshahara mkubwa wa fowadi huyo wa Napoli. (Corriere dello Sport - In Italian)


Beki wa kulia wa Newcastle Kieran Trippier huenda akaelekea katika moja ya klabu zinazovutiwa nchini Saudi Arabia, huku beki huyo wa zamani wa Uingereza mwenye umri wa miaka 33 akitaka kuondoka katika klabu hiyo ya Kaskazini Mashariki. (Sun).

Newcastle wamepuuza mapendekezo kwamba Trippier anataka kuondoka katika klabu hiyo na kuhamia Saudi Arabia au Uturuki. (Sportsport)

Winga wa zamani wa Chelsea na Fulham Willian, 36, amesafiri kwa ndege hadi Athens huku Olympiakos wakiwa na nia ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil. (Fabrizio Romano)

Sevilla inaonekana kupunguziwa bei ya kumnunua fowadi wa Uholanzi Memphis Depay, 30, ambaye anavutia Ulaya baada ya kuondoka Atletico Madrid. (Marca - in Spanish}

Mshambulizi wa Uingereza Ivan Toney, 28, atalipwa £403,000 kwa wiki - sawa na £800,000 kwa wiki kabla ya kutozwa kodi nchini Uingereza - baada ya kuhamia Al-Ahli, kutoka Brentford. (Mirror)

Beki wa Newcastle na Ireland Kaskazini Jamal Lewis, 26, anakaribia kuhamia klabu ya Brazil ya Sao Paulo (Belfast Telegraph)

.

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,

Roma wanakaribia kumnunua mlinzi wa Uhispania Mario Hermoso, 29, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Atletico Madrid msimu wa joto. (La Gazzetta dello Sport - in Italian.

Fowadi wa Oxford Mark Harris, 25, bado yuko kwenye rada za timu mpya katika ligi ya Bundesliga Holstein Kiel, ambayo ilijaribu kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales msimu huu wa Kiangazi (Sun),

Roma pia wako kwenye mazungumzo ya kumsajili beki wa kati wa zamani wa Ujerumani na Borussia Dortmund Mats Hummels, 35, huku wakitafuta kuchukua nafasi ya beki wa zamani wa Uingereza Chris Smalling, 34, ambaye anaelekea katika klabu ya Saudi Pro League Al-Fayha. (Sky Sports Italia)

Post a Comment

0 Comments