BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA USAJILI DUNIANI 10 SEPTEMBA 2024

 Manchester United huenda ikamnunua Eberechi Eze msimu wa joto, Liverpool pia wanamtaka winga huyo wa Crystal Palace, Chelsea wanataka kumwachilia David Datro Fofana kwenda Ugiriki.



Manchester United inamfuatilia winga wa Crystal Palace Eberechi Eze , 26, na huenda ikamtafuta mshambuliaji huyo wa Uingereza msimu ujao. (Manchester Evening News)

Liverpool wanaweza pia kumnunua Eze ikiwa fowadi wa Misri Mohamed Salah, 32, hatasaini mkataba mpya na klabu hiyo. (Liverpool Echo)

Chelsea wanatarajia kumuuza mshambuliaji wa Ivory Coast David Datro Fofana, 21, kwa klabu ya Ugiriki ya AEK Athens - dirisha la uhamisho la Ugiriki lipo wazi hadi Jumatano.(The Athletic - Usajili unahitajika)

th

Meneja wa zamani wa Chelsea na Tottenham Mauricio Pochettino anatarajiwa kuthibitishwa kuwa meneja mpya wa Marekani baada ya kukutana na wakuu wa soka wa Marekani. (Mail)

Manchester United wana nia ya kumuachilia winga wa Brazil Antony kwa mkopo huku Fenerbahce wakiwa katika nafasi nzuri ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24.(Sun)

Galatasaray wana nia ya kumsajili beki wa Tottenham na Wales Ben Davies mwenye umri wa miaka 31 kabla ya dirisha la uhamisho la Uturuki kufungwa tarehe 13 Septemba. (Takvim, kupitia Football Insider)

th

Kiungo wa kati wa zamani wa Chelsea John Obi Mikel alijaribu kumshawishi mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 25, kujiunga na The Blues kabla ya uhamisho wake wa mkopo kutoka Napoli hadi Galatasaray majira ya kiangazi . (Talksport)

Beki wa zamani wa Real Madrid na Uhispania Sergio Ramos huenda akakaribia kujiunga na klabu ya Brazil ya Corinthians . Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 amekuwa hana klabu tangu alipoondoka Sevilla majira ya joto. (Itatiaia - kwa Kireno)

th

Mahitaji ya mshahara ya kiungo Adrien Rabiot, 29, ni makubwa mno kwa Manchester United kumsajili Mfaransa huyo, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Juventus . (Football Insider)

Juventus bado wako tayari kupokea ofa kwa kiungo wa kati wa Brazil Arthur Melo, 28, ambaye anataka kusalia na kupigania nafasi yake katika klabu hiyo. (Fabrizio Romano)

Mshambulizi wa Kanada Jonathan David, 24, yuko kwenye mazungumzo kuhusu mkataba mpya na Lille lakini anaendelea kuhusishwa na kuhamia Ligi Kuu ya England .(Teamtalk)

Post a Comment

0 Comments