BETI NASI UTAJIRIKE

TAIFA STARS: TUPO TAYARI KUWASAMBARATISHA GUINEA

 Kikosi cha timu ya Taifa ,Taifa Stars kimejiandaa vyema kuelekea mchezo wa pili wa kundi H dhidi ya Guinea utakaopigwa hii leo majira ya saa 1;00 jioni huko Ivory Coast. Stars inapaswa kushinda mchezo huo mgumu ili kujiweka nafasi nzuri kwenye kundi lake linaloongozwa na DR Congo wenye alama 6 katika michezo miwili waliyocheza wakifuatiwa na Tanzania wenye alama 1 sawa na Ethiopia wenye alama moja na Guinea wakiburuza mkia.



Stars inakwenda kwenye mchezo huo ikiwa na wachezaji wazoefu,wenye vipaji na damu changa. Awali wadau walilalamikia kikosi cha kocha Hemed Suleiman wakimtaka awarejeshe kikosini Mbwana Samatta na Saimon Msuva ambao hawakuitwa hapo awali wakati taifa stars ikipata sare ya 0-0 mchezo uliopigwa dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Kuelekea mchezo huo kocha na kapteni walitoa maoni yao na kusisitiza wako imara kuwakabili wapinzani wao. Uwepo wa Amri Kiemba na  Jamhuri kihwelo wakiwasaidia Juma Mgunda na Hemedi Suleiman unaongeza hali ya ubora wa benchi la ufundi kuelea mchezo huo muhimu.

Lejendari Himid mao amenukuliwa akisema

''Wachezaji wote tuna deni la kuhakikisha tunafuzu AFCON2025, sote tunajua ladha ya michuano ile na hakuna kinachotuogopesha zaidi kupambana kwenye mchezo wetu dhidi ya Guinea na michezo mingine yote inayofuata. Tunawafahamu wapinzani wetu ni timu nzuri lakini tutapambana mpaka dakika ya mwisho kuhakikisha tunapata ushindi''

Naye kocha mkuu wa muda Bw.Hemedi Suleiman amenuuliwa akisema

'' Timu iko vizuri na hakuna majeraha kwa mchezaji yeyote, Tumejiandaa vyema na kurekebisha makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo wa awali. naamini tutakwenda AFCON 2025 kwa sababu tuna timu nzuri na mimi nina uzoefu na mashindano hayo nikiwa kama kocha msaidizi nyakati zote timu ilipofuzu.''

Post a Comment

0 Comments