Suarez ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Uruguay, akiwa amefunga mabao 69 katika mechi 142 akizidiwa na Diego Godin pekee aliyecheza mechi 161 nyingi zaidi za La Celeste.
Mshambuliaji huyo aliisaidia Uruguay kufika nusu fainali ya Kombe la Dunia la mwaka 2010 na kushinda taji lake la 15 la Copa America mwaka 2011, akitajwa kuwa Mchezaji Bora wa Mashindano huku akifunga mabao manne likiwemo la kwanza katika fainali - ushindi wa 3-0 dhidi ya Paraguay
Suarez atacheza mechi yake ya mwisho ya kimataifa huku timu ya Marcelo Bielsa ikiendelea kukusanya alama 13 kwenye michezo sita ya kwanza katika mchakato wa kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa ukanda wa CONMEBOL.
"Nimekuwa nikifikiria kuhusu hili na kulichambua hili. Ninaamini huu ni wakati mwafaka," Suarez aliyekuwa akitokwa na machozi alisema.
"Nataka nitulie nitakapocheza mchezo wangu wa mwisho na timu ya taifa. Nitakuwa na shauku ya kucheza kama nilivyokuwa mwaka 2007 nilipoichezea timu yangu ya taifa kwa mara ya kwanza.Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 19 sasa ni mchezaji mkongwe, mchezaji mzee, hata hivyo nataka kuijita mwenye historia ya ajabu nikiwa na timu ya taifa, ambayo nimetoa maisha kwa ajili ya timu."
KUKMBUKUMBU INAYOISHI KWA SUAREZ
Suarez alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa mpira wa mkono kwenye mstari wa goli na kuinyima Ghana bao la ushindi huku La Celeste ikishinda robo fainali ya Kombe la Dunia 2010 kwa mikwaju ya penalti, huku akikosa michuano ya Copa America 2015 baada ya kufungiwa mechi tisa kwa kumng'ata Giorgio Chiellini kwenye Kombe la Dunia la 2014.
"Tulipitia nyakati ngumu. Kulikuwa na nyingi,Binafsi, ilikuwa mbaya zaidi kwangu baada ya kosa langu kubwa mnamo 2014.Lakini hakuna kitu ambacho ningelaumu."
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 alicheza kwa muda mchache wakati Uruguay ilipotwaa medali ya shaba kwenye Copa mwaka huu, na kucheza mechi nne akitokea benchi huku Darwin Nunez akiongoza safu ya ushambuliaji.
Suarez alifunga bao la dakika za lala salama na kuipelekea Uruguay kwenye mchujo wa kuwania nafasi ya tatu kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Canada naUruguay ilishinda 4-3 kwenye mikwaju iliyofuata.
Ana mabao 16 katika mechi 20 za MLS alizochezea Inter Miami mwaka huu, huku Christian Benteke na Cristian Arango pekee (17 kila mmoja) wakiwa mbele yake katika mbio za Kiatu cha Dhahabu.
0 Comments