Cristiano Ronaldo anasema hana nia ya kustaafu soka la kimataifa .Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39 anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi na kufunga mabao mengi zaidi katika michuano ya kimataifa kwa wanaume akifunga mabao 130 katika michezo 212.
Hata hivyo, mustakabali wa Ronaldo ulitiliwa shaka baada ya kampeni zisizoridhisha za Euro 2024 ambapo alishindwa kutinga wavuni katika mechi tano na hiyo ilikuwa ni michuano ya sita ambayo Ronaldo ameshiriki, ikiwa ni rekodi, na kuwa mchezaji wa kwanza wa Ulaya katika historia kucheza mechi 50 kwenye mashindano makubwa.
“Wakati ukifika, sitaendelea,Hautakuwa uamuzi mgumu kufanya.Nikihisi sichangii chochote, nitakuwa wa kwanza kuondoka.Kwa sasa sijali chochote kilichosemwa wakati wa michuano ya Euro na Kombe la Dunia kwa sababu matarajio ya mashabiki yalikuwa makubwa kuhusu timu yao.Ujio wangu katika timu ya taifa ni kushinda Ligi ya Mataifa ya ulaya kwa sasa atumeshinda mara moja, na tunataka kushinda tena.
Fowadi huyo mwenye uhakika wa nafasi yake katika kikosi cha Ureno kwenye mechi za Ligi ya Mataifa dhidi ya Croatia na Scotland atakuwa na kazi moja tu kufunga bao la 900 katika maisha yake ya soka. Ronaldo aliongeza
0 Comments