BETI NASI UTAJIRIKE

NI WAKATI WA KIBWANA SHOMARI KUONDOKA YANGA?

 Baada ya kusajiliwa Attohoula Yao msimu uliopita ,Beki wa kulia wa Yanga alinukuliwa akisema kuwa kazini kwake kuna kazi kutokana na ushindani mkubwa na kiwango alichoonyesha Yao hadi kuingia kikosi cha kwanza.Namuangalia Kibwana ambaye amepoteza nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha Yanga kutokana na ubora wa full back Attohoula Yao, lakini hata anapokosekana Yao mara kadhaa kocha anaamua kuanza na Dickson Job kama mlinzi wa kulia badala ya Kibwana.


Benchi halijawahi kumfanya mchezaji akawa bora zaidi ya kushusha kiwango, Yanga ushindani ni mkubwa Kibwana ana kazi ya kufanya kwenye kikosi cha wananchi ili awe mbadala  sahihi hata pale ambapo anapokosena Yao Attohoula. Ubora wa Dickson Job na Yao Kwasi utaendelea kumfanya nyota huyo kutokuwa na uhakika wa nafasi ya kucheza kwa msimu huu.

Kama Kibwana atataka kukilinda kiwango chake na kuongeza thamani ya kimkataba basi anapaswa kufanya mambo mawili tu akiwa na jezi ya Yanga.Kwanza anatakiwa kumshawishi mwalimu gamondi kwa kujituma mazoezini na  kuanza kikosi cha kwanza lakini cha pili ni kama atashindwa kuwika mbele ya Yao basi atafute timu nyingine bora atakayopata uhakika wa namba.

Post a Comment

0 Comments