Klabu ya Namungo imefuta uvumi wa kumfukuza kazi kocha wake mkuu Mwinyi Zahera. Taarifa zisizo rasmi zilizagaa zikisema klabu hiyo imeachana na Zahera kwa kuwa na mwenendo mbaya baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo ya ligi dhidi ya Tabora United na Fountain gates.
Namungo wamekanusha taarifa hizo kwa kusema kocha huyo bado yupo Sana klabuni hapo na ameongezewa kocha msaidizi Ngawina Ngawina atakayesaidiana na Shadrack Nsajigwa. Kocha huyo aliingia matatani baada ya aliyekuwa mtendaji mkuu wa klabu hiyo kuondoshwa klabuni hapo.
0 Comments