Klabu ya Dodoma jiji imetangaza kumrejesha aliyekuwa Afisa Habari wake Moses Mpunga akichukua nafasi ya Patrick Semindu aliyerudishwa halmashauri ya jiji la Dodoma. Mpunga aliondoshwa katika nafasi hiyo baada ya kuhamishiwa wizara ya Ardhi na sasa amerejea rasmi kuchukua nafasi hiyo.
Moses Mpunga atakuwa afisa habari wa Dodoma jiji kwa msimu wa 2024/25 timu ikiwa chini ya kocha mkuu Meck Mexime. Aidha timu hiyo imecheza mechi 2 za ligi kuu ikipoteza mchezo mmoja kwa bao 1-0 dhidi ya Mashujaa FC na sare ya bila kufungana dhidi ya Pamba Jiji .
Mwezi Septemba Dodoma Jiji itacheza michezo minne ya Ligi kuu ya NBC Dhidi ya Namungo na Simba SC (mechi za nyumbani ) na ugenini itacheza dhidi ya Fountain Gates na Tanzania Prisons. Mpaka sasa Dodoma jiji hawajaweka wazi ni uwanja gani watautumia kwa mechi za nyumbani baada ya uwanja wa Jamhuri Dodoma kufungiwa.
0 Comments