Simba inaendelea kujipanga kuwang’oa Waarabu wa Libya Al Ahli Tripoli, mabosi wa klabu hiyo wana akili nyingine kubwa na bilionea Mohammed Dewji ‘MO’ amewafanyia umafia wa maana watani wao Yanga kwa kumchukua winga mmoja hatari.
Kwa mujibu wa Mwanaspoti ni kwamba winga Mkongomani, Ellie Mpanzu yupo hapa nchini atika hoteli moja kubwa iliyopo katikati ya Jiji, amekuja kumalizana na mabosi wa Simba ili dirisha dogo likifunguliwa aliamshe Msimbazi.
Mpanzu alihitajika zaidi na Simba dirisha kubwa la usajili, lakini alipokea mualiko wa kwenda Ubelgiji akaikacha ofa ya Simba, lakini baada ya majaribio yake kufeli huko amejikuta anaiwaza zaidi Simba kuliko kitu chochote.
0 Comments