BETI NASI UTAJIRIKE

MGUNDA HAKUPASWA KUACHWA NA SIMBA

 Klabu ya Simba imetangaza kumalizana na aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya Simba Queens Juma Mgunda. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Simba inasema mkataba wa kocha huyo na Klabu hiyo umemalizika na hawajamuongezea mkataba . Mgunda ameitumikia Simba SC kwa nyakati tofauti kama kocha mkuu wa muda kwa msimu wa 2021/22 .



Msimu wa 2022/23 alikuwa kocha msaidizi chini ya Robertinho na baadaye alipelekwa Simba Queens akiisaidia timu hiyo kutwaa  kombe la ligi kuu ya wanawake Tanzania msimu wa 2023/24  na kushika kufika nafasi ya nne kwenye michuano ya CECAFA kufuzu ligi ya mabingwa Afrika. Kwa sasa Simba iko chini ya kocha Mussa mgosi aliyekuwa kocha msaidizi chini ya mgunda .

Taarifa kutoka Simba 

Juma Mgunda ni kocha msaidizi wa timu ya Taifa la Tanzania akisaidiana na Hemed Suleiman 'MOROCCO' .Kocha Mgunda alikuwa anawaniwa na Namungo FC mwanzoni mwa msimu huu.

Je Mgunda alipaswa kuondoka Simba?

Post a Comment

0 Comments