Mabao mawili dhidi ya Real Betis yamefanikiwa kuondoa ukata wa mabao kwa mshambuliaji mpya wa Real Madrid, Kylian Mbappe. Nyota huyo wa kifaransa alijiunga na miamba hiyo ya soka duniani mwezi Julai akitokea PSG kama mchezaji huru.
Mbappe alifanikiwa kufungia Real Madrid goli lake la kwanza dhidi ya Bayern Leverkusen mchezo wa UEFA Super cup na kutwaa Kombe hilo.Hiyo ilikuwa mechi yake ya kwanza klabuni hapo.
Ukata wa mabao La Liga
Mbappe alifanikiwa kuanza mechi 3 za awali za La liga lakini alishindwa kufunga bao wala kutoa usaidizi wa mabao. Nyota huyo alianza kushutumiwa na wapinzani wake baada ya kushindwa kuisaidia madrid ilipopata alama mbili katika michezo miwili.
Mabao mawili aliyofunga dhidi ya Betis yameanza kurudisha imani kwa mashabiki wake na mabao hayo yameisaidia Madrid kufikisha alama nane ikishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi wakiongozwa na Barcelona wenye alama 12 kwenye michezo minne walizocheza.
0 Comments