BETI NASI UTAJIRIKE

MAJERAHA YAMPONZA FODEN

 Phil Foden huenda asijiunge na kikosi cha Uingereza kwa ajili ya mechi zijazo za Ligi ya Mataifa Ulaya kwa sababu ya majeraha.Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amecheza dakika 45 pekee msimu huu dhidi ya Chelsea wiki mbili zilizopita.


Mchezaji huyo alitajwa katika kikosi cha kocha wa muda wa Uingereza Lee Carsley kwa ajili ya mechi zao za Ligi ya Mataifa ya daraja la pili dhidi ya Jamhuri ya Ireland na Finland.

"Sidhani hivyo kwa sasa,Nadhani hatakwenda lakini sijui. Hajisikii vizuri. Lakini timu za taifa, ndizo zinazoamua." alinukuliwa Guardiola

Foden ameichezea England mechi 41 na alianza mechi zake zote kwenye Euro 2024.Uingereza itamenyana na Jamhuri ya Ireland mjini Dublin mnamo 7 Septemba (17:00 BST) na Finland kwenye uwanja wa Wembley mnamo 10 Septemba (19:45).

Post a Comment

0 Comments