Aliyekuwa kocha mkuu wa KenGold SC Fikir Elias na msaidizi wake Luhaga Mkunja wameachana rasmi na Timu hiyo baada ya kuanza vibaya ligi kuu ya NBC msimu wa 2024/25. Timu hiyo imepoteza michezo yote mitatu iliyocheza na kudondokea nafasi ya 15 sawa na Namungo FC iliyocheza michezo mitatu na kupoteza yote.
Kwa mujibu wa Kengold Makocha hao wameamua kubwaga manyanga na nafasi yao imechukuliwa kocha Jumanne Charles.Ken Gold yenye makazi yake jijini Mbeya ilipanda daraja msimu huu baada ya kufanya vizuri ligi ya Championship. Wengi waliamini ujio wa timu hiyo ungeleta chachu kwenye ligi lakini mambo yalianza kwenda kombo baada yakupokea kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Singida Black Stars mchezo uliopigwa dimba la Sokoine ,Ikafungwa mabao 2-1 na FountainGates na imefungwa 1-0 na KMC.
Tetesi za awali zinasema makocha Jamhuri Kihwelo na Juma Mgunda mmoja wao anaweza kutua Klabuni hapo
Hii ni barua iliyotolewa na ken gold
0 Comments