Taifa stars imejiandaa vyema kuelekea mchezo wake wa kwanza wa kufuzu michuano ya AFCON 2025 dhidi ya Ethiopia .Mchezo huo utapigwa Septemba 4 Dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam majira ya saa 1;oo usiku. Timu hiyo chini ya kocha wa muda Hemed Suleiman akisaidiana na Juma Mgunda itaanza kampeni hizo kwa mechi mbili mfululizo na kama itapata matokeo chanya basi itajiwekea mazingira mazuri ya kwenda Morroco mwaka 2025.
Kikosi cha timu ya Taifa kimeundwa na wachezaji 23. Wachezaji 20 wanatoka ligi kuu ya NBC na wachezaji 3 wanatoka ligi mbalimbali za nje ya nchi.Himid Mao ndiye mchezaji mkongwe kuliko wote kikosini na anaweza kuwa kapteni wa timu hiyo. Klabu ya Yanga imefanikiwa kutoa wachezaji 7 kwenye kikosi hicho wakifuatiwa na Azam FC wenye wachezaji 5 na Simba wametoa wachezaji 3.
Kikosi cha Kocha Hemed Suleiman kimekuwa na mabadiliko makubwa kwa nyota wengi wapya kuingia kikosini na baadhi ya wakonge kutoitwa kuelekea mechi hizo mbili. Mbwana Samata,Saimon Msuva,Kibu Denis na Aishi Manula wamekosekana kikosini na wachezaji wapya waliotwa ni Yona Amos,Abdulmalik Zakaria na Abel Josiah akitokea TDS TFF ACADEMY.hii hapa orodha ya wachezaji walioitwa timu ya taifa
0 Comments