BETI NASI UTAJIRIKE

ISHU YA MWENDA NA SINGIDA YAFIKA PABAYA FIFA WAKITAJWA

Baada ya klabu ya Singida Black Stars kumtaka Israel Mwenda kambini wakidai kumlipa kiasi cha shilingi milioni 160 Kati ya milioni 200 ya ada ya usajili,Mchezaji huyo ameonekana kuikataa barua hiyo na amesema yupo tayari kuvunja mkataba na klabu hiyo baada ya singida kushindwa kufikia makubaliano ya kimkataba.

 Nyota huyo amenukuliwa akisema.

Nipo kwenye mchakato wa kuvunja mkataba, nyie subirini mtapata taarifa, Singida wapo nje ya makubaliano tuliyokubaliana.

“Mpira wetu una changamoto sana. Halafu baadae utasikia wazawa wana matatizo,

“Nitaenda wapi sababu dirisha limefungwa? Hela niliyonayo inanitosha kuishi hata misimu minne bila kucheza mpira, kiufupi ni kwamba sina timu.”


Post a Comment

0 Comments