Kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum ameendelea kufanya kweli ligi kuu ya NBC baada ya kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya KMC mchezo uliopigwa Dimba la KMC COMPLEX jijini Dar es salaam. Katika mchezo huo Feisal alihusika katika mabao matatu akitoa pasi mbili za mabao kwa Iddi Nado pamoja na Lusajo Mwaikenda huku bao lililofungwa na Nathaniel Chilambo akihusika kulisuka.
Feisal aliibuka nyota wa mchezo huo kwa mara ya kwanza tangu ligi ya msimu wa 2024/25 uanze. Nyota huyo alikuwa bora zaidi msimu wa 2023/24akitengeneza nafasi 6 na kufunga mabao 19 katika mechi 30 aliyoichezea Azam FC. Kwa sasa bado anakandarasi ya miaka miwili ya kuitumikia Azam na baadhi ya timu zimeanza kumnyemelea zikihitaji huduma yake ikiwemo Simba na Yanga.Ubora anaouonyesha Feisal unazidi kumuongezea thamani yake sokoni na klabu anayoitumikia.
Je Azam imeanza kurejea kwenye ubora wake
Azam FC imecheza mechi 3 za Ligi kuu ya NBC.Mchezo wake wa kwanza walipata sare ya 0-0 dhid ya JKT Tanzania,mchezo wa pili walipata sare ya 0-0 dhidi ya Pamba JIJI na Mchezo wa tatu wameibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya KMC wakijikusanyia alama 5 katika michezo 3. Kikosi cha Azam kinaonekana kuanza kurejea kwenye ubora wake chini ya kocha mpya Rachid Taoussi na marengo yao kwa msimu huu ni kutwaa taji la ligi ya NBC na CRDB.
Mwalimu Rachid hakufanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi kilichopata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya KMC akianza na Foba Golini,mabeki wakiwa ni Lusajo Mwaikenda Nathaniel Chilambo Fuentes na Yoro Diaby,Eneo la kiungo liliundwa na Adolf Mtasingwa na James Akaminko,Pascal Msindo na mbele yao walisimama Feisal Salum ,Nassor Saadun na Idi Nado.
Azam iko katika nafasi ya kwenye msmamo wa ligi ikiachwa alama 7 na Singida Black Stars wanaoongoza ligi.
0 Comments