BETI NASI UTAJIRIKE

CAF:KILA TIMU INAOGOPA KUKUTANA NA YANGA

 Hakuna timu yoyote inayotamani kupangwa na Young African hatua za makundi kutokana na uwezo mkubwa waliouonyesha mechi 4 za kufuzu hatua za makundi. Yanga wamefuzu hatua hizo kwa kishindo baada ya kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 17-0 kwenye mechi hizo.



Raundi ya kwanza Yanga walipangwa na Vital'o ya Burundi na waliifunga timu hiyo jumla ya mabao 10 kwa raundi zote mbili. Mzunguko wa pili Yanga ilipangwa na CBE ya Ethiopia mchezo wa kwanza Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0 na mchezo wa pili uliopigwa uwanja wa New Amaan Stadium waliibuka na ushindi wa mabao 6-0.

Ubora wa Yanga uko wapi?

Yanga ni timu iliyokamilika kila idara kwa sasa. Kila mchezaji anayepata nafasi ya kucheza anaonyesha ubunifu na uwezo mkubwa. Ukitazama safu ya ulinzi inayoundwa na Dickson Job,Nikison Kibabake Ibrahim Baka, Boka,Kwasi Yao ,Mwamnyeto na mdaka mishare Djigui Diara imeifanya safu hiyo kuwa imara haswa baada ya kucheza mechi 4 za kufuzu hatua ya makundi na kuto ruhusu bao lolote na hata ukirejea nyuma utagundua mechi 6 walizocheza hivi karibuni wameruhusu bao 1 pekee dhidi ya Azam FC mchezo wa fainali ya kombe la ngao ya jamii.

Safu ya kiungo inayoundwa na Khalid Aucho,Mudathir Yahya,Clatous Chama ,Maxi Nzengeli ,Aziz Ki ,Pacome Zouzoua na Jonas Mkude imekuwa mwiba mkali kwa wappinzani wa Yanga . Nyota hawa wametengeneza mabao,wamefunga mabao na wamehusika kuzuia mipango ya wapinzani wao. Mwalimu Gamondi amekuwa akifanya mabadiliko ya wachezaji mara kwa mara wa eneo hilo na hakuna udhaifu unaoonekana.

Prince Dube na Clement Mzize ndiyo wauwaji tegemezi wa Yanga ,Clement ameendelea kuonyesha makali yake tangu kusajiliwa kwa Dube .Nyota hawa wamekuwa wazuri sana kumalizia pasi za mabao zinazotengenezwa na akina Chama,Pacome na Boka. Kwa sasa Yanga hawana tatizo la mshambuliaji ukizingatia uwepo wa Jean Baleke anayetegemewa kujiunga na timu hiyo mwezi Januari wakti wa dirisha dogo.

Chama na safari mpya jangwani 

Wakati wa ujio wa Chama ndani ya Yanga wengi walimtabiria kutofanya vizuri kutokana na staili ya kiuchezaji ya Yanga haiendani na namna Chama anavyocheza. Nyota huyo hakuanza kuingia moja kwa moja kikosi cha kwanza bali alikuwa akianzia benchi ,ubora wake katika mechi chache alizocheza umemmfanya nyota huyo kuwa chaguo la kwanza la Gamondi. Mara zote Gamondi amekuwa akimtumia Chama mara zote anapotaka soka safi na mabao.

Mchezo dhidi ya Vitalo ulimfanya chama aimbwe na mashabiki wa Yanga baada ya kufunga bao moja akitengeneza mengine 4 katika ushindi wa mabao 6-0. Mchezo wa duru ya pili dhidi ya CBE Chama alifunga bao 1 katika ushindi  wa mabao 6-0 na katika mchezo huo alionyesha kiwango kikubwa sana.

 

Post a Comment

0 Comments