Historia imeandikwa na nchi ndogo ya San Marino ikipata ushindi wao wa kwanza kabisa wa mechi ya kiushindani.Ushindi pekee wa awali wa San Marino ulikuwa ni wa mechi ya kirafiki dhidi ya Liechtenstein miaka 20 iliyopita, na waliwashinda wapinzani wao hao 1-0 shukrani kwa Nicko Sensoli aliyefunga bao la dakika ya 53, na kuibua shangwe kali.
Mabingwa wa Ulaya Uhispania walilazimishwa sare ya bila kufungana na Serbia mjini Belgrade, huku Uswizi wakiwa na Nico Elvedi na Granit Xhaka kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwenye kichapo cha 2-0 kutoka kwa Denmark.Patrick Dorgu alifunga bao la kwanza dakika ya 82, huku Pierre-Emile Hojbjerg akiongeza la pili kufuatia Xhaka kutolewa nje kwa kadi ya pili ya njano.
Kwingineko, mshambuliaji wa Newcastle Alexander Isak alifunga mabao mawili katika ushindi wa 3-1 wa Uswidi dhidi ya Azerbaijan, Slovakia iliilaza Estonia 1-0 na Bulgaria ya wachezaji 10 ikatoka sare ya 0-0 na Belarus.
0 Comments