BETI NASI UTAJIRIKE

AHMED ALLY: TUNAKWENDA KUWAONYESHA UBAYA UBWELA AL AHLI

 Kikosi cha Simba kimeanza safari kuelekea Libya kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa tarehe 15 Septemba dhidi ya Al Ahli Tripoli.Simba inapaswa kushinda mchezo huo ili kutengeneza mazingira mazuri ya kufuzu michuano ya Shirikisho kwa hatua ya makundi. Kikosi cha Simba kimeondoka Alfajiri ya leo na wachezaji wote ambao hawakuitwa timu za taifa na wale waliopo kwenye timu za mataifa yao wataungana na timu huko Libya.


Msemaji wa Simba Ahmed Ally amenukuliwa akisema ” Kikosi kimeondoka kupitia uturuki na tutapumzika nchini humo mpaka tarehe 12 kisha tutaelekea Tripoli Libya ambako tutafika tarehe 13 na tutaanza mazoezi mpaka tarehe 14 na 15 ndiyo siku ya mchezo wenyewe,Kikosi kitarejea Dar es salaam tarehe 18 kujiandaa na mchezo wa marudiano . Safari inajumuisha kikosi cha wachezaji 22 waliokamili pamoja na benchi la ufundi.”

Ahemed Ally aliongeza kwa kusema ”Mpinzani wetu Al Ahli Tripoli amejipanga msimu huu ukiangalia matokeo aliyoyapata siku za hivi karibuni pamoja na usajili aliofanya unaona amedhamiria kufanya ubaya ubwela kwenye kombe la Shirikisho lakini kwa bahgati mbaya anakwenda kukutana na wenye ubaya ubwela wenyewe  tumejiandaa kikamilifu kukabiliana naye kwenye mchezo huo mgumu na muhimu kwetu”

Post a Comment

0 Comments