Timu ya Taifa ya Congo DRC imeendelea kufanya vizuri michuano ya kufuzu AFCON 2025 baada ya kuibvuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ethiopia. Kwa sasa Congo anaongopza kundi H akiwa na alama 6 baada ya michezo miwili akifuatiwa na Tanzania wenye alama m0ja. Katika mchezo huo Bongonda alikuwa wa kwanza kutupia nyavuni dakika ya 62 na Fiston Mayele alipachika bao la pili dakika ya 76.
Michezo mingine iliyopigwa ni Uganda wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Congo na kuifanya timu hiyo kuongoza kundi K kwa alama 4 ikifuatiwa na Congo wenye alama 3. Madagascar walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Comoros mchezo wa kundi A, Lesotho wakifungwa nyumbani bao 1-0 na Morocco mchezo wa kundi B .
Mchezo mgumu ulikuwa ni kundi E ukiwakutanishga Equatorial Guinea na Togo mchezo uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.Niger na Ghana walitoka sare ya 1-1 mchezo wa kundi F pamoja na Angola kushinda mabao 2-1 mchezo wa kundi hilo. Ushindi wa Angola unaifanya timu hiyo kuwa na alama 6 ikifuatiwa na sudan wenye alama 3.
0 Comments