Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya NBC ,Young Africans wameanza vyema kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar .Mchezo huo uliopigwa dimba la kaitaba mkoani Kagera na Yanga walipata bao la kwanza kupitia kwa Maxi Nzengeli dakika ya 44 akimalizia pasi kutoka kwa Pacome Zouzoua . kipindi cha kwanza kilimalizika Yanga wakiongoza kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili kocha Miguel Gamondi alifanya mabadiliko ya wachezaji kwa kuwapa nafasi Clement Mzize aliyefunga bao la pili na kukamilisha ushindi wa mabao 2-0. Wachezaji wengine walioingia kwenye mchezo huo ni Clatous Chama na Musonda. Mbali na Kagera Sugar kupoteza mchezo hiyo haikumzuia mchezaji Nassoro Kapama kuondoka na tuzo ya mchezaji bora wa mechi kwa kuonyesha kiwango kizuri.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga kupanda kutoka nafasi ya 12 hadi ya nne wakiwa na alama tatu na mabao 2 ya kufunga wakati Kagera Sugar ikiendelea kufaya vibaya kwa kupoteza alama 6 kwenye michezo miwili waliyocheza wakishika nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC sawa na Namungo waliopoteza mchezo wao dhidi ya Fountain Gates.
0 Comments