Brentford wanashikilia bei wanayotaka kumuuza Ivan Toney, Ajax wanafikiria kumnunua Aaron Ramsdale, Real Madrid hawatapokea ofa zozote kutoka Saudi Arabia kwa Vinicius Junior.
Brentford wanashikiliakuwa pauni milioni 60 ndio gharama ya kumnunua mshambuliaji wa England Ivan Toney, 28, ambaye anafuatiliwa na Chelsea na Manchester United(Independent)
Ajax wana nia ya kumsajili kipa wa Arsenal Muingereza Aaron Ramsdale, 26. (Sky Sports).
Real Madrid haitamruhusu mshambuliaji wa Brazil Vinicius Junior, 24, kuondoka kwenda Saudi Pro League hata kama watapokea ada ya kuvunja rekodi ya dunia. (AS - kwa Kihispania.
Al-Ittihad hawataki kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa N'Golo Kante, 33, licha ya kuhusishwa na West Ham na Atletico Madrid(Fabrizio Romano
Bournemouth inamlenga mshambuliaji wa Arsenal Muingereza Eddie Nketiah, 25, ili kuziba pengo la Dominic Solanke kuelekea Tottenham (Mail)
Brighton wamemtafuta mlinzi wa Ufaransa Olivier Boscagli, 26, lakini PSV Eindhoven wanataka zaidi ya walichotoa Seagulls (Eindhovens Dagblad - kwa Kiholanzi)
Leicester City wametoa ofa ya £4m kwa fowadi wa Crystal Palace na Ghana Jordan Ayew, 32. (Mail)
Barcelona imekataa ofa ya Everton ya pauni milioni 23.9 ikijumuisha nyongeza ya malipo kwa mshambuliaji wa Brazil Vitor Roque mwenye umri wa miaka 19 (Sky Germany)
Manchester United wana nia ya kumsajili beki wa zamani wa Chelsea na Uhispania Marcos Alonso, 33 , ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Barcelona . (Athletic -Usajili unahitajika)
Beki wa Wales Ben Davies, 31, huenda akakamilisha mwaka wa mwisho wa mkataba wake na Tottenham badala ya kutafutauhamisho msimu huu wa joto. (Football Insider)
Napoli na RB Leipzig wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid Mhispania Samu Omorodion mwenye umri wa miaka 20 baada ya uhamisho wake kwenda Chelsea kukosa kufanyika (Football Insider)
Getafe wana nia ya kumchukua kwa mkopo beki wa kati wa Tottenham Muingereza Ashley Phillips, 19. (Sky Sports)
Vilabu viwili vya Premier League vimefanya uchunguzi na Southampton kuhusu kupatikana kwa kiungo wa kati wa Argentina Carlos Alcaraz, 21. (Teamtalk)
Brentford wanakaribia kukamilisha dili la beki wa kati wa Jamhuri ya Ireland Dara O'Shea, 25, ambalo litaipa Burnley faida ya pauni milioni 7 walizolipa kumsajili kutoka West Bromwich Albion mwaka jana. (Telegraph - usajili unahitajik
0 Comments