Klabu ya Tabora United imepewa onyo na TFF kuacha mara moja kushirikiana na aliyewahi kuwa mkurugenzi wa Kitayosce FC na mwenyekiti wa Chama cha Soka TAbora BW.Yusuph Kitambi.
Kamati ya Maadili ya TFF ilimfungia maisha Bw.Yusuf Kitambi pamoja na Ulimboka Mwakingwe kutojihusisha na soka baada ya kukutwa na kosa la upangaji wa matokeo wakati Kitayosce FC ikicheza na Fountain gates mchezo wa championship mwaka 2023 April 16. Hukumu hiyo ilitoka mwezi Mei 2023.
TFF imeionya TABORA UNITED kupitia barua ya wazi kutoshirikiana na Kitambi na yeyote atakayeshirikiana naye atakutana na rungu la shirikisho hilo.
0 Comments