BETI NASI UTAJIRIKE

SIMON JORDAN AMPA TAHADHARI BELLINGHAM

 Simon Jordan anaamini Timu ya Taifa Uingereza si mahali salama kwa Jude Bellingham. Mmiliki huyo wa zamani wa Crystal palace na mchambuzi wa Talk Sports amenukuliwa akisema vyombo vya Habari na wadau wa soka ndiyo chanzo cha wachezaji wadogo wa kiingereza kushindwa kufanya vyema. 



Simon anasema wachezaji wengi wa Uingereza wameingizwa kwenye mtego na watu wasio sahihi kwa kuwaaminisha Vitu vikubwa ambavyo wachezaji wale hawana na matokeo yake ni wachezaji kupoteza mwelekeo na viwango vyao. Mchambuzi huyo amesema

Wachezaji ambao ndio dili la kweli pia watapata uzito kupita kiasi. Jude Bellingham atazidi kuzidiwa. Itakuwa ni msalaba usiovumilika kwake kuubeba, kwa sababu hatimaye hatafikia viwango ambavyo watu wanamjenga.

"Ni tatizo kubwa ndani ya soka la Uingereza. Tunawapa wachezaji wachanga sana, haraka sana. Huo ndio mwanzo wa mwisho kwa baadhi yao kwa sababu wanazunguka na watu wasio sahihi na kuwasikiliza. Wamezidiwa kupita kiasi, wanaanza kuamini kila kitu ambacho kila mtu anasema juu yao na wanaacha kujifunza.

Post a Comment

0 Comments