Simba Queens imepoteza mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu michuano ya CECAFA kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kawempe Muslim Ladies FC kwa mabao 2-0. Matokeo hayo yanaifanya Simba Queens kurejea nchini bila medali yoyote. Michuano hiyo inafanyika nchini Ethiopia na bingwa wa mchezo huo atafuzu moja kwa moja kushiriki ligi ya mabingwa Africa. Timu zilizofuzu fainali ni CBE women ya nchini Ethiopia na Kenya Police Bullets.
Simba Queens ilianza vyema michuano hiyo kwa kuongoza kundi ikishinda mechi mbili na sare moja wakijikusanyia alama saba. Mchezo wa nusu fainali uliwakutanisha Simba Queens waliopoteza kwa mabao 3-2dhidi ya Kenya Police bullets. Mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu Simba Queens imeambulia kipigo cha mabao 2-0 na kuifanya timu hiyo kufungwa jumla ya mechi 2 kati ya 5 walizocheza.
Kikosi cha Simba Queens kinachoongozwa na kocha Juma Mgunda kilianza na Gelwa Yonah,Fatuma Issa,Wincate Kaari,Ruth Ingosi,Violeth Nicholaus,Mary Saiki,Elizabeth wambui,Ritticia Nabbosa,Jentrix shikangwa,Vivian Corazone na Asha Djafari. Kikosi hicho kinautofauti na kile kilichoanza dhidi ya Kenya Bullets kwa baadhi ya wachezaji akiwemo Caroline Rufa,Daniela Ngoyi,Precious Christopher na Amina Bilali.
0 Comments