Cristiano Ronaldo ameendelea kuweka rekodi ndani na nje ya uwanja. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Sporting Lisbon,Manchester United ,Real Madrid Juentus na sasa Al Nasry amefanikiwa kuweka rekodi kwenye mitandao ya kijamii baada ya kufikisha wafuasi milioni 14.6 kwenye mtandao wa Youtube.
Cristiano alijiunga na Youtube tarehe 21 agosti 2024 na kuweka video 19. Mpaka sasa ameweza kujipatia tuzoya dhahabu ya Youtube baada ya kufikisha wafuasi milioni 1 ndani ya masaa mawili. Kwa mwenendo huo inatabiliwa ronaldo atafikisha wafuasi milioni 100 ndani ya mwezi mmoja.Kwa sasa Ronaldo ndiye mwenye wafuasi wengi zaidi wa mtandao wa Instagram akifikisha wafuasi milioni 636.
0 Comments