Mchezo wa Kwanza wa ligi kuu ya NBC msimu wa 2024/25 umemalizika kwa sare ya bila kufungana ukizikutanisha Pamba JIJI dhidi ya Tanzania Prisons.
Mchezo huo umepigwa dimba la CCM KIRUMBA na ulijaa ufundi mwingi kwa timu zote mbili,mashabiki wa Pamba jiji wamefurahishwa kwa namna ambavyo timu yao imeanza vizuri msimu huu wakimpongeza golikipa Yona Amos kwa kutwaa tuzo ya mchezaji Bora wa mchezo huo.
Pamba wamepanda daraja msimu huu baada ya kushuka daraja kwa miaka 23.Timu hiyo ilishuka daraja mwaka 2001 ikitwaa Pamba Football club na ilipopanda daraja ilibadili jina na kuitwa Pamba jiji ikisimamiwa na Manispaa ya jiji la Mwanza.
Vikosi vilivyoanza kwenye mechi hiyo
0 Comments