BETI NASI UTAJIRIKE

MBAPPE ATWAA KOMBE LA KWANZA REAL MADRID

 Kylian Mbappe alihitaji dakika 69 pekee kutwaa Kombe lake la Kwanza la UEFA . Nyota huyo amefanikiwa kutwaa Kombe akiwa na jezi ya Real Madrid baada ya klabu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Atlanta kwenye mchezo wa UEFA Super cup uliowakutanisha mabingwa wa ligi ya mabingwa ulaya (real Madrid) dhidi ya mabingwa wa Europa league (Atlanta) kwa msimu wa 2023/24.Mbappe alisajiliwa na Real Madrid kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na PSG.



Tathmini ya mchezo 

Kocha Ancelloti hakuwa na mabadiliko makubwa ya kiuchezaji na machaguo ya wachezaji katika mchezo huo. Eneo la ulinzi liliongozwa na Tibout ,militao,carvajal,f Mendy na Rudiger. Eneo la kiungo liliundwa na Tchouameni,Bellingham na valverde huku eneo la ushambuliaji liliundwa na Mbappe ,Vinicious jr na Rodrigo akitumia mfumo wa 4-3-3.

Dakika ya 58 Valverde alipokea pasi kutoka kwa Vinicious jr na kufanikiwa kuandika bao la kwanza.Dakika ya 69 Kylian alipokea pasi kutoka kwa Bellingham na kuandika bao la pili lililowahakikishia Real Madrid Kombe Hilo.kila mchezaji alionyesha ubora na thamani ya kuvaa jezi ya Real Madrid.

Ushindi huu unamaana gani kwa Mbappe

Huu ni mchezo wa kukumbukwa zaidi kwa Mbappe kwani hakuwahi kutwaa Kombe lolote la UEFA .Akiwa ndani ya real Madrid amefanikiwa kutwaa Kombe Hilo kirahisi zaidi tena katika mchezo wake wa Kwanza.

Kisaikolojia inamwongezea ujasiri wa uthubutu na tutegemee matokeo chanya kwenye msimu wake wa Kwanza La Liga na michuano y UEFA


Post a Comment

0 Comments