Klabu ya Real Madrid imeanza kutetea ubingwa wa La Liga kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Real Mallorca. Madrid walikuwa wa Kwanza kupata bao dakika ya 13 kupitia kwa Rodrigo aliyemalizia pasi ya Vinicious jr.
Real Mallorca walisawazisha bao hilo kupitia kwa Muriqi dakika ya 53 kipindi cha pili. Matokeo hayo yameipeleka Real Madrid katika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi na huu ni mwanzo mgumu kwa timu hiyo kulinganisha na wapinzani wao Barcelona walioshinda mchezo wake wa Kwanza na kuongoza ligi
Kocha Ancelotti aliwapa nafasi vijana wake kwa kuunda Safu hatari ya ushambuliaji iliongozwa na Vinicious jr, Rodrigo,Mbappe. Safu ya kiungo ililindwa na Tchouameni, Valverde na Bellingham na eneo la ulinzi liliongozwa na Rudiger,Militao ,Dan Carvajal na Fellan Mendy aliyepewa Kadi nyekundu dakika ya 90+3.
0 Comments