Aliyewahi kuwa mshambuliaji Bora wa Yanga msimu wa 2022/23 Fiston Mayele ameiongoza timu ya Pyramids kuisambaratisha JKU ya Zanzibar kwa mabao 6-0 .JKU na Pyramids zinawania kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Africa na mchezo huo wa awali raundi ya Kwanza umepigwa nchini Misri.
Mayele aliiandikia Pyramids bao la kuongoza dakika ya 8,bao la pili lilifungwa na El Karti dakika ya 15, Lasheem aliweka bao la tatu dakika ya 27 na Adel alipachika bao la nne dakika ya 32. Mchezo huo ulikwenda mapumziko kwa Pyramids kuongoza kwa mabao 4-0.
Kipindi cha pili Lasheem alirejea tena kambani na kufunga bao la 5 dakika ya 55 huku Zalaka akishindilia bao la 6 dakika ya 88. Matokeo hayo yanawafanya JKU kuwa na mwanzo mbaya wa michuano hiyo na watatakiwa kushinda mabao 7-0 kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa tarehe 26 Agosti.
0 Comments