BETI NASI UTAJIRIKE

KMC COMPLEX YAANZA KUVUNA MAMILIONI YA SIMBA

 Klabu ya Simba SC imeuchagua uwanja wa KMC COMPLEX kutumika kwa mechi za nyumbani za ligi kuu ya NBC. Simba imelazimika kutumia uwanja huo baada ya uwanja wake wa nyumbani Benjamin Mkapa kuwa kwenye marekebisho makubwa na umefungwa kwa sasa.

Simba itacheza mechi 15 za Ligi ya NBC kwenye uwanja huo na taarifa za ndani zinasema kila mchezo utailazimu Simba kulipa kiasi cha shilingi milioni 6 ili iweze kuutumia uwanja huo wenye uwezo wa kubeba mashabiki 6000. Mpaka sasa Simba imeutumia uwanja huo kwenye mchezo wa ligi  dhidi ya Tabora United mchezo uliomalizika Simba kushinda mabao 3-0

Uwanja huo wa kisasa uliopo Mwenge jijini Dar es salaam unamilikiwa na Manispaa ya Kinondoni inayomiliki klabu ya KMC FC. Uwanja huu unatumika nyakati za mchana pekee na kuna uwezekano ukawekwa taa hivi karibuni ili uweze kutumika nyakati zote.

Amospoti imejipanga kufanya mazungumzo na meneja wa uwanja huo ambao ulituimika wakati wa michuano ya Dar Port Kagame Cup.


Post a Comment

0 Comments