BETI NASI UTAJIRIKE

KISA AWESU AWESU TFF YAIPIGA SIMBA BITI

 Klabu ya KMC imefanikiwa kushinda kesi ya uhalali wa mchezaji Awesu Awesu  aliyetambulishwa na Simba hivi karibuni. Klabu hiyo ilipeleka malalamiko TFF kupinga uhamisho wa mchezaji huyo wakidai  bado wanamkataba naye na klabu ya Simba haikupeleka ofa yoyote kwa klabu hiyo.


Hukumu iliyotolewa na TFF inasema mchezaji huyo ni mali halali ya KMC na Simba wameonywa kwa kutofuata taratibu pindi wanapomtaka mchezaji yeyote. Kwa upande mwingine klabu hiyo imekumbwa na sintofahamu kwenye masuala ya usajili likiwemo suala la Kibu Denis,Lameck Lawi,Israel Mwenda na Aishi Manula.

hii hapa barua ya TFF



Post a Comment

0 Comments