Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amebakiza mwaka mmoja wa kuutumikia mkataba wake ndani ya klabu hiyo. Arteta alijiunga na Arsenal kuwa kocha mkuu mwaka 2019 akitokea Manchester City alikokuwa kocha msaidizi wa Pep Guardiola. Kocha huyo amekuwa na mwendelezo mzuri wa kuiboresha timu hiyo .
Mafanikio ndani ya Arsenal
Arteta mwenye miaka 42 amefanikiwa kuiongoza Arsenal kutwaa mataji matatu ambayo ni Kombe la FA 2019/20 na Makombe mawili ya ngao ya jamii msimu wa 2020/21 na 2023/24. Kocha huyo ameiwezesha Arsenal kumaliza nafasi ya pili kwenye michuano ya ligi kuu Uingereza mara mbili mfulilizo na msimu wa 2023/24 aliweza kutoa wachezaji watano kwenye kikosi bora cha msimu.
Arteta anatumia mfumo wa 4-3-3 na amefanikiwa kuiongoza Arsenal katika mechi 233 akishinda mechi 138 sare 38 na kufungwa mechi 57 sawa na asilimia 59.23 za ushindi.
Mipango baada ya msimu wa 2024/25
Mpaka sasa si Mikel Arteta wala uongozi wa klabu umesema lolote kuhusiana na hatma ya kocha huyo anayemaliza mkataba wake mwezi june 2025. Pande zote zinaonekana kuridhishwa na mwenendo wa timu na kuna uwezekano kocha huyo akaendelea kuinoa timu hiyo. Arteta amekuwa na matumizi mazuri ya pesa za uSajili na kuifanya klabu hiyo kutumia kiasi cha paundi milioni 590 toka mwaka 2019 hadi 2023.Mfano wa mchezaji aliyepandishwa thamani na kocha Mikel Arteta ni Bukayo Saka aliyenunuliwa mwaka 2020 kwa dau la paundi milioni 7 na kwa sasa thamani yake imepanda mpaka kufikia paundi milioni 140.
Arteta ameongeza thamani ya kikosi cha Arsenal kwa kukiwezesha kikosi hicho kufikia thamani ya bilioni 1.17 na kuwa moja ya timu yenye kikosi cha thamani kubwa barani Ulaya.
0 Comments