BETI NASI UTAJIRIKE

DODOMA JIJI YAJA KIVINGINE KWA KUSHUSHA NYOTA 13

 Klabu ya Dodoma Jiji chini ya kocha Mecky Mexime imeonyesha nia ya kuleta ushindani mkaIi msimu wa 2024/25  kwa sajili walizofanya. Klabu hiyo ilimaliza nafasi ya 12 msimu uliopita na sasa imejipanga vyema kuchuana vilivyo  kwenye kinyang'anyilo cha makombe ya  NBC Premier League na kombe la shirikisho la CRDB.


Kwa msimu wa 2023/24 Klabu hiyo ilicheza michezo 30 ikishinda michezo 8 sare 9 na kupoteza michezo 13 wakikusanya alama 33 sawa na uwiano wa alama 1 kwenye kila mchezo waliocheza. Klabu hiyo ilionekana kuwa na matatizo kila sehemu baada ya kufunga mabao 19 pekee na kufungwa mabao 32 hivyo kuwa na uwiano wa magoli -13.

Kocha Mecky Mexime amepania kurejesha hadhi ya Dodoma jiji kwa msimu huu na tayari matokeo yameanza kuonekana kwa kuwaleta nyota mbalimbali wenye uwezo mkubwa na uzoefu wa ligi yetu. Usajili wa washambuliaji hatari  Laurent Lusajo  na Wazir Junior aliyeshika nafasi ya tatu kwa ufungaji wa magoli ligi ya NBC Wazir Junior msimu uliomalizika  ni ishara kwamba kocha anataka kuongeza makali kwenye safu ya ushambuliaji.Jina la kiungo Ajib nalo limeandikwa ndani ya Dodoma Jiji akitokea Coastal Union.

Mbali na wachezaji hao lakini pia Dodoma imeimarisha benchi lake la ufundi kwa kuwaleta Nizar Khalfan (kocha msaidizi), Peter Manyika (Kocha wa magolikipa) na Francis Mkanula (kocha wa viungo)

Hawa hapa nyota 10 waliosajiliwa na Dodoma Jiji  












Post a Comment

0 Comments