BETI NASI UTAJIRIKE

COASTAL UNION YAANZA VIBAYA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

 Klabu ya Coastal union imeambulia kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa FC Bravo mchezo wa raundi ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho. Coastal union waliambulia kipigo hicho nchini Angola.

FC Bravo walifunga mabao mawili kipindi cha Kwanza na bao la tatu walifunga dakika za lala salama za kipindi cha pili. Mchezo huo uliokuwa mgumu kwa wanamangushi na mbinu za kocha David Ouma ziligonga mwamba.

Coastal Union wamekuwa na mwenendo mbaya tangu walipotoka pre season Pemba.Timu hiyo ilikubali kufungwa mabao 5-2 na Azam Fc kwenye mchezo wake wa nusu fainali ya ngao ya jamii na walipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu wa michuano hiyo. Kufungwa mabao matatu na FC Bravo kunaifanya timu hiyo kuwa na rekodi mbaya ya kufungwa mabao 9 katika mechi 3 huku wao wakifunga mabao 2 pekee katika mechi hizo.

Mchezo wa marudiano dhidi ya FC Bravo utapigwa tarehe 25 jijini Dar es Salaam na Coastal Union watatakiwa kushinda mabao 4-0 jambo linalowezekana kwa kocha David Ouma.

Post a Comment

0 Comments