Manchester city wameanza vyema mbio za kutetea ubingwa wa ligi kuu Uingereza kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Chelsea. Bao la Kwanza liliwekwa kimiani na Halaand dakika ya 18 kipindi cha Kwanza na kiungo Kovacic aliandika bao la pili dakika ya 84.
Matokeo hayo yanawafanya Manchester city kushika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi na kuwaongezea morali kuelekea ubingwa wa tano mfululizo wa ligi hiyo.
Kocha Guardiola ameendelea kubadili mifumo ya kiuchezaji baada ya kuanzisha mabeki watatu mbele Yao viungo wawili ambao ni Kovacic na Lewis .Safu ya kiungo wa ushambuliaji iliundwa na wachezaji wanne ambao ni Kelvin de Bruyne , Bernardo Silva,Doku na Savio mbele yao akisimama Halaand kama mchezaji wa mwisho.
Msimu wa 2023/24 City wakitwaa ubingwa wa nne mfululizo wakiwa na alama 91. Msimu huo walipoteza mechi 3 pekee wakitoa sare mechi 7 na kushinda mechi 28. Kwa namna timu ilivyocheza ni wazi kwamba wamedhamilia kutetea ubingwa huo.
0 Comments