BETI NASI UTAJIRIKE

CHAMA ATUPIA YANGA IKIISAMBARATISHA VITAL'O

 Klabu ya Yanga imeanza vyema hatua za awali za michuano ya ligi ya mabingwa Africa kwa ushindi wa mabao 4 dhidi ya Vital'o ya nchini Burundi.

Bao la Kwanza la Yanga liliwekwa kimiani na Prince Dube dakika ya 6 .Mchezo huo ulikwenda mapumziko Yanga wakiongoza kwa bao 1-0.

Bao la pili liliwekwa kimiani na Clatous Chama dakika ya 68 akimalizia shuti la Aziz ki lililogonga mwamba. Clement mzize aliyetoka sub akichukua nafasi ya Prince Dube aliweka bao la tatu dakika ya 74 ya mchezo huo na Aziz ki alifunga bao la nne kwa mkwaju wa penati dakika ya 90

Mchezo huo wa mkondo wa kwanza umepigwa dimba la Azam Complex uwanja wa nyumbani wa Vital'o.Mchezo wa marudiano utapigwa dimba la Benjamin Mkapa siku ya jumamosi tarehe 22 agosti.

Klabu ya Yanga imeondoka na kiasi cha shilingi milion 20 kama zawadi kutoka kwa Rais Samia suluhu aliyeahidi kununua kila bao kwa shilingi milioni 5 kama timu itashinda

Post a Comment

0 Comments