BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA YAPATWA NA PIGO KUU

 Aliyewahi kuwa mwenyekiti na mfadhili wa klabu ya Yanga Yusuph Manji amefariki dunia hii leo akiwa nchini marekani. Taarifa zinasema bosi huyo wa makampuni ya Quality Group amefariki usiku wa kamkia leo akipatiwa matibabu.


Manji aliingia madarakani siku chache baada ya Yanga kuchapwa mabao 5-0 na Simba mei 6 mwaka 2012 na alifanya kazi kubwa kwa kuvunja makundi  mawili  yaliyokuwa yanatofautiana kiitikadi  ndani ya Yanga moja likiitwa Yanga Kampuni na jingine likiitwa Yanga asili.

Manji alihudumu ndani ya Yanga kwa miaka 5 toka mwaka 2012 hadi mwaka 2017 na kufanikiwa kuiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu mara 4 na timu hiyo kushiriki michuano ya kimataifa.

Manji anakumbukwa kwa sajili alizofanya enzi hizo akiwa mwenyekiki ikiwemo usajili wa Kamusako,Juma Kaseja,Obrey Chirwa ,Emanuel Okwi na Donald Ngoma. pia alifanikiwa kuleta makocha wa kiwango cha juu akiwemo Micho,Sam Timbe, Tom Santief Papic na Ernest Brandts.

Post a Comment

0 Comments