BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA YAMTAMBULISHA KIUNGO MKENYA

 Klabu ya Yanga imeendelea na zoezi la kutambulisha nyota wake wapya iliyowasajili hivi karibuni kuelekea msimu ujao. Klabu hiyo yenye makao yake makuu jijini Dar es salaam imefanikiwa kumsajili Duke Abuya kutoka Ihefu.

Nyota huyo anacheza safu mbili uwanjani akicheza kama kiungo mshambuliaji na winga ya kulia.Abuya akiwa na vilabu vya Ihefu na Singida alionyesha kiwango cha hali ya juu na kuwashawishi mabingwa hao kumsajili. Abuya anaungana na Clatous Chama,Aziz Ki,Mudathir Yahya na Pacome  katika eneo la kiungo.

Safari ya Duke Abuya

Duke Abuya alizaliwa mwaka 1994 nchini Kenya na mwaka 2015 alianza safari yake ya soka kwa kuitumikia mMathare Fc ya nchini humo,Msimu wa 16/17 alijiunga na Kariobang sharks na  baadaye kutimkia nchini Zambia kuitumikia Nkana FC ambako hakudumu na kuamua kurejea nchini Kenya na kujiunga na klabu ya Kenya Police na baadaye kuuzwa Singida Big Stars kisha Ihefu FC zote za Tanzania.

Nafasi yake katika timu ya taifa

Abuye amekuwa akiitwa mara kwa mara katika timu ya Harambee Stars. nyota huyu amekwishacheza michezo 30  tangu mwaka 2019 akiisaidia kenya kucheza Afcon na michezo ya kufuzu kombe la dunia na mataifa ya Africa

Je Yanga wamenufaika na usajili huu

Yanga wamenufaika na usajili wa Duke abuya kwa sababu mchezaji huyu anauzoefu wa kucheza ligi kuu Tanzania ,kiwango chake ni cha muendelezo na amekuwa na juhudi kila anapopata nafasi . Kwa nafasi anayocheza kuna nyota wengi wenye uwezo sawa naye hiyo itampa nafasi mwalimu Gamondi kuwa na kikosi kipana ikizingatiwa Yanga itashiriki michuano ya NBC Premier League, CRDB FA CUP NA LIGI YA MABINGWA AFRICA (caf champions league) hivyo kuwazungusha wachezaji haitakuwa kazi ngumu kwa kocha huyo.




Post a Comment

0 Comments