BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA YAFANYA KWELI AFRIKA KUSINI

 Klabu ya Young African iliyopo nchini Africa Kusini imeendelea vyema na maandalizi ya msimu wa 2024/25.Young Africans wamecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya TS GALAXY inayoshiriki ligi kuu Africa Kusini mchezo uliomalizika kwa Yanga kushinda bao 1-0.


Katika mchezo huo mshambuliaji mpya Prince Dube ndiye aliyefunga bao  na winga Max Nzengeli aliendelea kuonyesha uwezo mkubwa kama alivyofanya kwenye mchezo wa awali dhidi ya FC Augsburg.

Katika mchezo huo kocha Gamondi aliwaanzisha Mshery, mkude,Kibwana Shomary,Dickson Job,Aziz Andambwile,Jonas Mkude,Mdathiri Yahay,Salum Abubakar Sureboy,Shekhan, Denis Nkane,Clement Mzize na Farid Musa lengo ni kuwapima uwezo nyota hao na namna ambavyo atakiimalisha kikosi chake kuelekea msimu ujao.

Itakumbukwa Yanga watashiriki michuano mbalimbali msimu huu ikiwemo ligi ya NBC,Kombe la CRDB FA CUP,Kombe la Mapinduzi na michuano ya ligi ya mabingwa Africa. Mpaka sasa klabu hiyo imekwishasajili wachezaji mahili na wenye uzoefu akiwemo Clatous Chama ,Jean Baleke na Prince Dube.

Klabu hiyo itacheza mchezo wake wa mwisho wa kujipima tarehe 28 Julai dhidi Kaizer Chief nchini Afrika Kusini na itarejea nchini mwishoni mwa mwezi Julai ili kuhitimisha wiki ya Wananchi itakayofanyika uwanja wa Benjamini Mkapa  tarehe 4 Agosti 

Post a Comment

0 Comments